This archive report was first published on 16 July 2020.
Polisi wa Murang'a wamemkamata Naibu Chifu mmoja na kuanzisha msako dhidi ya mwenzake na polisi waliotoweka baada ya kudaiwa kumnajisi msichana wa shule.
Naibu Chifu na afisa wa polisi hao wanasema walimtega msichana huyo na kuingia naye msitu wa Aberdare ambapo walimnajisi.
Uchunguzi wa kina umeanzishwa kuhusu kisa hicho, na Kamanda wa polisi John Ngare alithibitisha kisa hicho.
Wenyeji hao walimnasa naibu mmoja wa chifu ambaye walimtandika kabla ya maafisa wa polisi kuwasili eneo hilo na kumkamata huku washukiwa wenzake wakitoweka vichakani.
Watatu hao wanaripotiwa kufumaniwa msituni na wenyeji wenye hamaki wakitekeleza tendo hilo la unyama mnamo Jumatano, Julai 15, 2020.