This archive report was first published on 16 July 2020.
COVID-19: Chuo Kikuu cha Nairobi Kuhusishwa na Kifo cha Wafanyakazi Wawili ¶
Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Stephen Kiama, amethibitisha kuwa wafanyakazi watatu wa chuo hicho walimalizwa na COVID-19.
Wahasiriwa hao walikuwa wakifanyia kazi zao nyumbani, huku wengine wawili wakigunduliwa kuwa na virusi hivyo.
Wizara ya Afya ilitangaza Jumatano, Julai 15, kuwa watu wengine 7 walifariki dunia kutoka na virusi hivyo, na kufanya idadi ya vifo kufikia 209.
Idadi ya walioambukizwa virusi vya COVID-19 sasa imefikia 11,252 baada ya watu wengine 461 kupatikana na virusi hivyo Jumatano Julai 15.
Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Stephen Kiama, amesema kuwa ni lazima wafanyakazi wote wafanyie kazi zao nyumbani, na wale wenye miaka 58 na zaidi wachukue likizo.
“Tunaendlea kusisitiza kuwa wafanyakazi wafanyie kazi nyumbani. Wale wenye miaka 58 na kuendelea wanaweza kuchukua likizo na kila mmoja ajiweke salama mahali popote alipo,” alisema Kiama.
Chuo Kikuu cha Nairobi kimefunguliwa kufunguliwa mnamo Septemba, pamoja na taasisi nyingine, kwa kuwa vyuo vikuu vinatazamiwa kufunguliwa tena.
Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Stephen Kiama. Picha: UGC.