Skip to main content

COVID-19 Outbreak in Machakos: 68 New Cases Recorded

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 15 July 2020.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amefichua kuwa wagonjwa 68 kati ya 97 wa COVID-19 waliorekodiwa Jumatano, Julai 15, 2020, kutoka Machakos wanafanya kazi katika kampuni moja.

Maambukizi mapya yalirekodiwa baada ya wizara ya afya kupima halaiki ya watu katika kampuni moja eneo bunge la Mavoko.

Gavana Mutua aliwahimiza wakazi kuendelea kuvalia maski na kunawa mikono.

Asilimia 90 ya visa vya corona vilivyorekodiwa kaunti ya Machakos vilithibitishwa eneo la Mavoko, alisema Gavana Mutua.

"Kwa sasa asilimia 90 ya visa vya kaunti ya Machakos vinatoka eneo la Mavoko- Athi River na Mlolongo. Wagonjwa wapya wote hawakuwa na dalili za virusi hivyo," alisema Mutua.

Idadi ya wagonjwa nchini Kenya iliongezeka na kufika 11, 252 kufikia Jumatano, Julai 15, 2020, baada ya Katibu Msimamizi wa Afya Rashid Aman kuthibitisha watu wengine 461 wameambukizwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →