This archive report was first published on 15 July 2020.
Barobaro ilizuka katika eneo la Kamunyolo huko kaunti ya Makueni baada ya mzee anayesemekana kuwa poifa ramli kumvamia lofa akimuonya dhidi ya kumtongoza binti yake.
Alipokamatwa na kigugumizi, mzee alikuwa na hasira kwa sababu alikuwa na mipango ya kumridhisha bintiye taaluma yake.
Alimkuta jamaa na kumzomea vikali na kumfuata kwake akimuonya akome kumtongoza msichana wake na kusambaratisha mipango aliyo nayo juu yake.
Alipofoka, mzee alisema, "Nimesema achana na msichana wangu. Koma hata kumpigia simu kabisa. Nikikuona naye tena walahi utakula nyasi. Hapo ndio utajua mimi ni mganga wa kweli,"
Alipokamatwa tena, jamaa alijitetea kwa kusema, "Mimi sijamtongoza msichana wako. Pengine mtu mwingine,"
Maneno ya lofa yalimpandisha mzee hasira na kumwambia jamaa, "Una ujinga sana wewe kijana. Wewe hutoshi kuoa kwangu. Huyu msichana wangu napanga kumwachia kazi yangu. Achana naye kabisa na umkome,"
Alipokubali kosa lake, jamaa alimueleza mzee, "Nimekubali mzee. Hutawahi sikia tena nikimtomgoza binti yako. Wewe endelea na mipango yako ya kumridhisha kazi yako,"
Alipomwacha, mzee alimua kurudi nyumbani na kuahidi kumwadhibu vikali jamaa iwapo atasikia ameonekana tena na bintiye popote.