This archive report was first published on 15 July 2020.
Julai 15, 2020: Idadi ya walioambukizwa na virusi vya COVID-19 nchini Kenya imeongezeka hadi 11,252 baada ya watu 461 kupatikana na virusi hivyo.
Wakati wa kuhutubia wananchi Jumatano, Julai 15, katibu wa wizara ya Afya, Rashid Aman, aliongeza kuwa watu 51 zaidi wamepona kutokana na virusi hivyo na wameruhusiwa kuondoka hospitalini.
Idadi ya wagonjwa waliopona kutokana na virusi hivyo kufikia sasa ni 3,068.
Wakati huo huo, Aman aliongeza kuwa watu wengine 7 wamefariki dunia kutoka na virusi hivyo na kufanya idadi ya vifo kufikia 209.