This archive report was first published on 15 July 2020.
Basi la Homeboyz ambalo liliwaua watu 55 lageuzwa lori la mizigo ¶
Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya alipakia picha akiidhinsha gari linaloonekana kuwa lori la mizigo ambalo lilikuwa na usajili sawa na basi la Homeboyz liliwaua watu 55 mnamo Oktoba 2018 katika eneo la Fort Ternan, Kericho.
Imeibuka kuwa mmiliki wa basi hilo, Cleophas Shimanyula, alibadilisha basi hilo kuwa Isuzu FVR kwa gharama ya KSh1,450 pekee.
Rekodi za Halmashauri ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (NTSA), zinaonyesha kuwa mnamo Juni 2019, Shimanyula alituma maombi ya kubadilisha muundo wa basi hilo lililohusika kwenye ajali pasi kubadilisha nambari ya usajili.
Shimanyula alitumia KSh300 kubadilisha hadhi ya gari hilo, KSh300, kubadilisha rangi ya basi hilo, KSh300 za kubadilisha mmiliki wa gari hilo, stakabathi zake akigharamia KSh500 na ada ya KSh50, ambapo gharama jumla ilikuwa KSh1, 450, kulingana na rekodi za NTSA.
Maombi yake yalikubalikan na kuidhinisha mnamo Januari mwaka huu na NTSA.
Na kutokana na mradi huo wa maji, huenda lori lake ndilo litatumika kubeba vifaa vya ujenzi wa mradi huo wa maji.