Skip to main content

Raymond Moi amesema kuwa yuko tayari kumrithi kaka yake Gideon Moi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 15 July 2020.

Raymond Moi amesema kuwa yuko tayari kumrithi kaka yake Gideon Moi

Raymond Moi, Mbunge wa Rongai, amesema kuwa yuko tayari kumrithi kaka yake mdogo Gideon Moi, katika kiti cha useneta Kaunti ya Baringo mnamo 2022.

Raymond alisema hivyo wakati wa mkutano wa hadhara eneo bunge lake, akizungumza siku ya wikendi.

Alidokeza kuwa Gideon atawania urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Raymond pia aliwarushia vijembe washindani wake wanaopania kumbwaga endapo atawania tena kiti cha ubunge kwa mara ya tatu mfululizo.

“Kwa hivyo baadhi ya watu wanafikiria wanaweza kuja na kuwania kiti dhidi yangu mwaka 2022. Waache kupoteza muda wao na rasilimali. Nitawashinda kama nilivyowashinda 2013 na 2017,” alisema Raymond.

Raymond wakati wa hafla ya mazishi ya Mzee Moi ambapo alimpokeza Gideon fimbo ya mamlaka. Picha: UGC.

Raymond alimpokeza Gideon fimbo ya mamlaka ya baba yake wakati wa mazishi ya hayati Daniel Moi.

Alipokeza fimbo hiyo kama njia ya kumpa baraka za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta wakati hatamu zake za uongozi zitakamilika mwaka 2022.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →