This archive report was first published on 14 July 2020.
Wafanyikazi 41 wa Pumwani Hospital wameambukizwa na COVID-19 ¶
Julai 14, 2020
Wafanyikazi 41 wa hospitali ya Pumwani wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona, kufichua Katibu wa Wizara ya Afya Patrick Amoth.
Amoth alisema visa hivyo 41 vilithibitishwa baada ya wafanyikazi 290 wanaohudumu katika kliniki ya akina mama kujifungua kupimwa.
Alisema hudumua katika kliniki hiyo zitaendelea kama kawaida akiongeza kuwa mikakati yote imewekwa sambamba ili kulinda afya ya wahudumu wa afya.
Wafanyikazi 100 katika kituo hicho cha afya wanapanga kupimwa baada ya kuibuka kwamba wauguzi 15 kutoka hospitali hiyo waliambukizwa virusi hivyo hatari.
Wauguzi hao hawakuonesha dalili zozote za kuugua virusi hivyo na kwamba hamna kisa chochote za maafa ya mgonjwa, kwa kauli ya Mwenyekiti wa Muungano wa Wauguzi Nchini (KNUN) Boaz Onchari.
Onchari alisema wauguzi hao hawakuonesha dalili zozote za kuugua virusi hivyo na kwamba hamna kisa chochote za maafa ya mgonjwa.