This archive report was first published on 14 July 2020.
Wiki iliyopita, Edith Nyasuguta Mochama, ambaye wengi walijua kama Nyasuu, alikuwa akivuka barabara katika mtaa wa Dallas mjini Texas, nchini Marekani, wakati aligongwa na lori.
Alikimbizwa katika kituo kimoja cha afya ambapo aliaga dunia Julai 9, 2020, akipokea matibabu.
Uchunguzi bado unaendelea, lakini familia ya Nyasuu, pamoja na marafiki wa karibu wanaoishi Marekani, wameanza mchango wa kugharamia kusafirishwa kwa mwili wake hadi humu nchini.
"Natumai mko salama, tunasikitika kuwatangazieni kifo cha ghafla cha Edith Nyasuguta Mochama aliyetambulika na wengi kama Nyasuu," alisema mmoja wa familia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.