Skip to main content

Mutahi Ngunyi: Mt Kenya Shabikia DP Ruto Ili Jiangamize Kisiasa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 14 July 2020.

Naibu Rais William Ruto amekuwa na mawimbi ya kisiasa baada ya ripoti za mwanya wa kisiasa kati yake na Rais Uhuru Kenyatta.

Mchanganuzi wa kisiasa Mutahi Ngunyi amesema eneo la Mlima Kenya lilifanya njama ya kumshabikia Naibu Rais William Ruto ili aanze kujiangamiza kisiasa.

Alisema hiyo ndiyo sababu Ruto amekuwa akionyeshwa uungwaji mkono katika eneo hilo tangu waungane na Rais Uhuru Kenyatta.

Alisema eneo hilo lilimshabikia kisiasa ili aweze kujichimbia kaburi lake la kisiasa kabla ya 2022.

Alisema eneo hilo lilikuwa likimuogopa DP na ndipo likaweka mikakati ya jinsi watamuangusha.

"Huku wakimhofia Ruto, mikakati ya GEMA ilikuwa kumshabikia na kisha kumuangusha. Mara tu ambapo huanzia jambo kutoka juu ni wakati ambapo unachimba shimo," alisema Ngunyi.

Ujumbe wa mchanganuzi huyo ulizua hisia mseto kwenye mtandao wa twitter.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →