This archive report was first published on 14 July 2020.
Matumaini ya Man United ya kusonga hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu yalivunjwa baada ya kulazimishiwa droo ya 2-2 na Southampton ugani Old Trafford.
Mechi hiyo ilikuwa ya Jumatatu, Julai 13 usiku, na Man United walilazimika kutafuta bao ili kuwa kifua mbele baada ya Stuart Armstrong kufungua ukurasa wa mbao katika dakika ya 12.
Marcus Rashford alidhania kuwa alifungia United bao la kufutia machozi kunako dakika ya 16 dakika chache baada ya kuwasiliana na Anthony Martial lakini juhudi zake zilikataliwa.
Anthony Martial alifunga bao lingine dakika tatu baadaye huku akiweka kimyani kombora lililompita James McCarthy na kumalizia vyema pasi ya Bruno Fernandes.
Walakini, mabao kutoka kwa Rashford na Martial hayakutosha kukomboa United dhidi ya kumaliza droo ugani Old Trafford.
Obafemi alitinga dakika za lala salama na kuhakikisha kuwa mechi hiyo inakamilika sare huku kikosi cha Manchester kikishikilia nafasi ya tano.
Awamu ya pili iliwashuhudia Saints wakitumia vizuri nafasi ya United kulaza damu na kuadhibu vijana wa Ole Gunnar Solskjaer huku Obafemi akifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho.