This archive report was first published on 14 July 2020.
Madaktari waliogunduliwa kuwa na COVID-19 wajiuzulu Sudan Kusini ¶
Wizara ya afya nchini Sudan Kusini imetangaza kuwa wafanyakazi 16 wa afya ambao waligunduliwa kuwa na virusi vya corona wamejiuzulu.
Wahudumu wanane walijiuzulu wiki jana kutokana na kushinikizwa na familia zao ambazo zilikuwa na wasiwasi kuwa watapeleka virusi hivyo nyumbani na kuwaambukiza jamaa zao.
Profesa Mayen Machut Achiek, ambaye anasimamia jopo kazi la COVID-19, alisema kuwa wanane hao ni ikiwemo wanne wa usafi na wauguzi wanne.
Profesa Machut Achiek alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi walikuwa wamegundua kuwa wameogopeshwa na namna wagonjwa wa COVID-19 walivyokuwa wakiangamia, na hivyo kusita kuripoti kazini.
Profesa Machut Achiek aliahiid kuwa serikali ya Sudan Kusini itatoa vifaa vya kujilinda kwa wahudumu wa afya.
Wizara ya afya ya Sudan Kusini inasema kuwa hospitali zote za nchi hiyo zimeathirika na hali hii, na kuwa watarejea kufanya kazi baada ya kupokea vifaa vya kujilinda.
Waziri wa afya wa Kenya, Mutahi Kagwe, ametangaza kuwa watu wengine 12 wamefariki dunia kutokana na virusi vya COVID-19.
Kenya kwa sasa imerekodi vifo 197 kwa jumla na visa 189 vipya vya maambukizi vimeripotiwa.