Skip to main content

Wauguzi 15 wa Hospitali ya Pumwani Wanasa COVID-19

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 13 July 2020.

Wauguzi 15 wa Hospitali ya Pumwani Wanasa COVID-19

Julai 13, 2020

Wauguzi 15 wa hospitali ya Pumwani wameambukizwa virusi vya coronavirus, kuhusisha wasiwasi wa usalama wa wahudumu wa afya.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wauguzi Nchini (KNUN) Boaz Onchari amethibitisha hayo na kuelezea wasiwasi wake kuhusu usalama wa wahudumu wa afya.

Onchari alisema wauguzi hao hawakuonesha dalili zozote za kuugua virusi hivyo na kwamba hamna kisa chochote za maafa ya mgonjwa.

Onchari alisema, "Siwezi sema idadi kamili ya wahudumu wa afya katika hospitali hiyo ambayo wameambukizwa maradhi hayo. Lakini naweza tu kuzungumza kwa niaba ya wauguzi na kuthibitisha 15 kati yao wameambukizwa virusi hivyo," kulingana na ripoti ya Nairobi News.

Onchari alisema ni jambo la kusikitisha kwa sababu wauguzi hao walipata maambukizi kutoka wadi ya akina mama kujifungua.

Haya yanajiri wakati nchi inaomboleza kifo cha daktari wa kwanza kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo nchini Kenya.

Daktari huyo, Doreen Lugaliki, alikuwa daktari wa kwanza kuangamizwa na coronavirus. Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 38 na alitajwa na wenzake kama daktari mwenye bidii aliyejitolea kazini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →