This archive report was first published on 13 July 2020.
Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vya wapenzi wawili ambao miili yao ilipatikana ikiningi'nia kwenye paa la nyumba.
Wapenzi hao wanasemekana walikuwa wakiishia katika mtaa wa Kayole jijini Nairobi kabla ya kusafiri mashinani baada ya Rais Uhuru Kenyatta kufuangua mipaka ya kaunti Julai 6.
Imesemekana kuwa wawili hao walikuwa wamesafiri kutoka Nairobi hadi kijiji cha Kaumoni kata ya Nguluni kaunti ya Machakosi Jumapili, Julai 12.
Wapenzi hao wanasemekana walikuwa Dennis Pius mwenye umri wa miaka 28 na Susan Ndeto mwenye umri wa miaka 19.
Polisi hawajabaini iwapo wawili hao waliuana au kuna mwenye alimua mwenzake kabla ya kujiua.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.