This archive report was first published on 13 July 2020.
Manchester City ina uhakika wa kumaliza kati ya vilabu bora Ligi Kuu msimu huu na wanaweza kuongeza Kombe la FA na UEFA licha ya kupoteza taji la nyumbani.
Uamuzi huo ulitolewa Jumatatu, Julai 13, na uliondolea klabu hiyo mashtaka ya kuvunja sheria za kudhibiti fedha inazotumia kutoka kwa udhamini kipindi cha mwaka 2012 na 2016.
Uamuzi huo ulisikizwa mnamo Juni kupitia video kabla ya uamuzi kutolewa.
Uamuzi huo unatazamiwa kuwapiga City jeki katika kivumbi cha vilabu nne bora, huku mahasidi wao wakipigania tiketi ya kushiriki mtanange huo.
Chelsea, Man United na Leicester City ni miongoni mwa timu ambazo ziko mbioni kupata nafasi katika mashindano hayo ya Bara Uropa.