This archive report was first published on 12 July 2020.
Paul Pogba, mchezaji wa kikosi cha Manchester United, amekuwa na majeraha ya uso baada ya kugongana na Victor Lindelof wakati wa mazoezi.
Alionyesha majeraha hayo kupitia Instagram, huku akimpongeza Lindelof kwa uledi wake kwenye safu ya ulinzi.
Alisema, "Victor uliniangamiza! Angalia hii kaka. Mungu Wangu! Hii ndio hutokea ukikutana na jamaa wa barafu Victor Lindelof," huku akionyesha jeraha ndogo kwenye mdomo wake wa juu.
Alionyesha pia kuwa amekuwa akishirikiana vyema na Bruno Fernandes katika safu ya kati, na sasa anatazamia kusalia Old Trafford baada ya msimu huu.
Manchester United, ambao wameandikisha matokeo bora wanapania kurejea uwanjani siku ya Jumatatu, Julai 13, wakati watakapokuwa wakigarazana na Southampton ugani Old Trafford.