Skip to main content

Hatimaye Rais Donald Trump avalia barakoa kwa mara ya kwanza hadharani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 12 July 2020.

Trump Avalia Barakoa Hadharani Kwa Maradufu

Rais Donald Trump alijitokeza akiwa amevaa barakoa hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona nchini Marekani.

Alipowatembelea wanajeshi waliojeruhiwa na wahudumu wa afya katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed, Julai 11, Trump alikuwa amevaa barakoa.

Alipowasili Ikulu ya White House, Trump alikanusha madai ya awali kuwa alipinga uvaaji wa maski na kuelezea kuwa anaamini zina muda wake.

"Sijawahi kamwe kupinga uvaaji wa barakoa, lakini ninaamini kuwa zina mahali na muda wake," alisema Trump huku akiondoka.

Trump alikuwa amevalia maski nyeusi iliyopigwa muhuri wa rais katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed.

Aliongeza kuwa hana shida kuvalia barakoa maeneo ya umma ila atafanya hivyo kwa kupenda kwani kulingana naye suala hilo halitakani kuwa la lazima nchini humo na maeneo mengi watu hukaa kwenye umbali mkubwa.

Trump alidai kuwa kufunika uso hakuhitaji kuwa suala la lazima katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Ukiongozi huyo ambaye amekuwa kwenye mstari wa mbele kupinga maagizo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kuvalia barakoa hadharani, alijitokeza na maski nyeusi iliyopigwa muhuri wa rais.

Idadi ya vifo vya virusi vya corona nchini Marekani ilipanda hadi 800 kila siku, ikikaribia 135 000.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →