Skip to main content

Wagonjwa wengine 278 waongezeka, idadi yagonga 9,726

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 11 July 2020.

Wagonjwa wengine 278 waongezeka, idadi yagonga 9,726

Idadi ya sampuli zilizopimwa tangu virusi vya corona kutua nchini Machi 2020 imefika 207, 987, kufikia Jumamosi, Julai 11.

Watu 99 wamepata nafuu kutokana na COVID-19, na kufikisha idadi ya waliopona kutimia 2,832.

Wagonjwa watatu aidha walifariki dunia katika saa 24 zilizopita na kupandisha idadi ya waliongamizwa 184.

Jimbo la Kwale liliandikisha wagonjwa 139 ambao kwa sasa wote wamepata nafuu isipokuwa 9 ambao wanaduhumiwa wakiwa manyumbani mwao.

Katibu wa Afya Mercy Mwangangi alitoa mashine za ventileta kupiga jeki serikali ya jimbo hilo kupambana na maambukizi.

Gavana wa Kwale Salim Mvurya aliwahakikishia wakazi serikali yake imetenga vitanda 340 vya kuwatenga wagonjwa wa homa hiyo kulingana na maagizo ya serikali.

Wakati huo Mvurya alitoa shukrani zake kwa wizara ya afya kwa kushirikiana nao na kuisadia katika kuthibiti maambukizi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →