This archive report was first published on 11 July 2020.
Polisi wa Bungoma wamepata mwili wa mama na wanawe wawili waliokwenda mtoni Nzoia Jumapili, Julai 5, baada ya siku tano za kujitafuta.
Winny Kulangwa, mama wa umri wa miaka 24, alishukiwa kuwatupa wanawe watatu wenye umri wa mwaka mmoja na miaka minne majira ya saa tatu usiku.
Chifu wa eneo hilo Kennedy Wamalwa aliiambia The Standard kuwa mwanawe mchanga alipatikana akiwa angali amefungwa katika mgongo wa mamake miili hiyo ilipopatikana.
Uchunguzi wa awali ulionesha kwamba mama huyo alitatizika kimawazo kufuatia ugomvi na mumewe, kwa kuwa familia ya Kulangwa ilisema kuwa marehemu hakuonesha matatizo yoyote ya kuzongwa na mawazo kabla ya kutenda kisa hicho.
Polisi wamehusisha mauaji hayo na mzozo wa kinyumbani.
"Tumekuwa tukiitafuta miili kwa siku tano. Ni afueni baada ya miili hiyo kupatikana kwani sasa polisi wataanzisha uchunguzi ili kubaini kilichompelekea mama kujitupa pamoja na wanawe mtoni," alisema Chifu Kennedy Wamalwa.