This archive report was first published on 11 July 2020.
Shule za Kibinafsi Zinazuiwa Kwa Kifedha Kwa Sababu ya COVID-19 ¶
Shule nyingi zilijikuta katika matatizo ya kifedha wakati taasisi za elimu zilifungwa kufuatia janga la COVID-19. Zaidi ya shule 100 huenda zikafungwa kabisa, na hilo litathiri zaidi ya wanafunzi 39,000.
Wanafunzi wataulia wakati wakifunzwa na mwalimu wao darasani. Picha: UGC.
Wanafunzi wataulia wakati wakifunzwa na mwalimu wao darasani. Picha: UGC.
Mwenyekiti wa shule za binafsi aliiomba serikali kuzipiga jeki shule hizo ili kuokoa jahazi. Alisema taasisi hizo za kibinafsi zinaajiri walimu 300,000 na tayari 158,000 kati yao wamepoteza ajira huku wengine wakitumwa kwa likizo la lazima.
"Shule hizo hazina pesa za kulipa kodi ya hadi 2021," mwenyekiti huyo aliaambia Citizen TV.
Hiyo ina maana kwamba mitihani ya kitaifa, Mtihani wa shule za msingi (KCPE) na ule wa shule za upili (KCSE), itafanyika 2021. Mwaka wa 2020 unasadikiwa umepotea sababu ya COVID-19 na wanafunzi wote wa shule za msingi na shule za upili, watarudia madarasa 2021. Mitihani ya kitaifa itafanywa baadaye mwakani (2021)," alisema Waziri wa Elimu George Magoha.