This archive report was first published on 10 July 2020.
Maafisa wa trafiki wameagizwa kutoweka vizuizi katika barabara kuu za jijini, sababu barabara nyingi zinatumika kuendeleza ufisadi.
Maafisa wa trafiki wakisimamisha gari.
Maafisa wa trafiki wamekuwa wakipiga kambi mahali pamoja na kama ilivyo ada, baadhi yao wanawahangaisha madereva na kuchukua mlungula kutoka kwao.
Maafisa wa trafiki wamesutwa mara kwa mara kuweka vizuizi barabarani kisha wanatumia fursa hiyo kuwahangaisha madereva.
Naibu Inspekta Generali Edward Mbugua amesema kuwa maafisa hao wanapaswa kuzunguka katika barabara kuu wakishika doria na wala sio kupiga kambi mahali pamoja.
Maafisa wa trafiki wamekuwa wakipuuza maagizo ya Inspekta Generali wa Polisi Hilary Mutyambai ambaye alisema vizuizi havipaswi kuweka barabarani.
Maafisa wa trafiki wanapaswa kuhudumu chini ya OCS na wala sio makamanda jinsi ambavyo imekuwa awali.