Skip to main content

Shule ya kifahari ya St Andrew's Turi imeripoti visa 18 vya Covid-19

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 10 July 2020.

Wasiwasi umetanda katika kijiji cha Turi baada ya watu 18 kupatikana na coronavirus Alhamisi, Julai 9.

Watu hao 18 ni wafanyakazi wa shule ya kifahari ya St Andrew Turi eneo bunge la Molo kaunti ya Nakuru.

Waziri wa Afya kaunti ya Nakuru Gichuki Kariuki amedhibitisha hayo na kusema wagonjwa hao ni kati ya wale 23 walioripotiwa Alhamisi.

Wakazi katika wadi ya Turi waliamkia wasiwasi baada ya taarifa kutamba kwenye mtandao kuwa janga la coronavirus limevamia kijiji hicho.

Wakazi wa eneo hilo wana wasiwasi kwamba wafanyakazi walio na virusi hivyo wanaishi shuleni humo na kuna uwezekano wa kuhusishwa na familia zao.

Shule hiyo inafaa kutengwa mara moja ili kuepuka maambukizi, kwa kusema mfanyibishara wa Turi Salaons Lempaa.

Waziri wa Molo Kuria Kimani aliwataka wakazi kuwa watulivu akiwahakikishia kuwa suala hilo linashughulikiwa na sekta ya afya.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →