This archive report was first published on 10 July 2020.
Jamaa asifiwa kwa ujasiri wake wa kuokoa maisha ya mtoto aliyerushwa kutoka kwa orofa ¶
Phillip Blanks, afisa mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani, alikuwa katika hatua ya kujitolea kwa maisha ya mtoto mchanga aliyerushwa kutoka kwa orofa tatu katika jumba lililokuwa linateketea eneo la Phoenix, Arizona, Ijumaa, Julai 3.
Blanks, ambaye alikuwa akiendesha mazoezini pamoja na swahiba wake, alisikia mayowe na kisha kukimbia kwenye makazi hayo ambapo alimuona mtoto huyo "akipepea angani" kama helikopta.
Alipofika kwenye makazi hayo, Blanks alikuwa na ujasiri wa kuokoa maisha ya mtoto huyo mwenye miaka mitatu. Alisimulia kwamba alikuwa na uwezo wa kumdaka mtoto huyo na kumuweka salama.
Blanks alisimulia, "Watu walikuwa wanapiga kamsa. Wakisema kuna watoto hapa na kuanza kuwatupa watoto chini. Nilimuona jamaa mmoja akiwa amesimama hapo tayari kumpokea mtoto huyo, lakini alionekana kana kwamba hakuwa na uwezo, kwa hivyo nikaingilia kati."
Video iliyopakiwa mtandaoni na shirika la ABC News inaonyesha Blanks akipiga mbizi kumdaka mtoto huyo mchanga na kumuweka salama.
Maafisa wa usalama wa Arizona Republic walitoa taarifa kwamba mtoto huyo pamoja na dada yake mwenye miaka minane wanauguza majeraha mabaya lakini mama yao aliangamia katika moto huo.
Blanks anasifiwa kwa ujasiri wake wa kuokoa maisha ya mtoto aliyerushwa kutoka kwa orofa tatu katika jumba lililokuwa linateketea eneo la Phoenix, Arizona.