Skip to main content

Kagwe Awaonya Waraibu wa Miraa Dhidi ya Kukaribiana

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2020.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa waraibu wa miraa wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa kupuuza agizo la kutotangamana.

Alisema hii Alhamisi, Julai 9, akiwa katika hospitali ya rufaa ya Coast General baada ya kuzuru na kukagua vituo vya afya mjini Mombasa.

Waziri Kagwe alisema waraibu wa miraa huonekana kufurahia zaidi stimu za mmea huo wakiwa wamekaribiana wakipiga gumzo.

Alisema, "Lakini mnapaswa kufahamu bado utamu ni ule ule tu hata mkichonga kama mmeketi mbali mbali," kwa hivyo waraibu wa miraa wanapaswa kutotangamana.

Wagonjwa wengine 733 waliripotiwa kupata nafuu huku vifo 56 zaidi vinavyotokana na virusi hatari vya corona vikirekodiwa.

Idadi ya wagonjwa 811 wa Covid-19 kutoka Mombasa wamelazwa hospitalini huku wengine 335 wakihudumiwa kutoka nyumbani.

Naibu Gavana William Kingi alisema licha ya kwamba Mombasa iko katika hatari zaidi ya kuenea kwa virusi hivyo, maambukizi yamekuwa yakipungua kwa siku za hivi karibuni.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →