Skip to main content

Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab wavamia kituo cha polisi cha Karokora

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2020.

Kituo cha polisi cha Karokora katika kaunti ya Garissa kilishambuliwa na wanamgambo wa kundi la al-Shabaab, lakini hakuna afisa wa polisi aliyejeruhiwa.

Wanamgambo hao zaidi ya 20 walikuwa wamejihami kwa silaha hatari na wanasemekana kuharibu mitandao ya mawaliano kabla ya kushambulia kituo hicho.

Maafisa wa polisi wamewataka wakazi wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya na Somalia kuwa macho kwani magaidi wamekuwa wakilenga maeneo hayo.

Uchunguzi zaidi unafanywa dhidi ya shambulizi hilo, na Mkuu wa Polisi wa Kusini Mashariki Rono Bunei amesema kwamba hakuna aliyepata majiraha kwenye shambulizi hilo.

"Hakuna aliyepata majiraha kwenye shambulizi hilo, lakini maafisa wetu wameanzisha msako kuwasaka washukiwa," alisema Rono.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →