Skip to main content

Muuguzi KNH, Mhudumu wa Hotelia Taabani kwa Kuunda Vyeti Ghushi vya COVID-19

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2020.

Muuguzi KNH, Mhudumu wa Hotelia Taabani kwa Kuunda Vyeti Ghushi vya COVID-19

Julai 9, 2020 - Muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, Delvine Enock Moses, na mhudumu wa hoteli, Samwel Shikanda, wamekabiliwa na mashtaka ya kuunda vyeti feki vya COVID-19.

Wawili hao walikabiliwa na mashtaka 11 ya kuunda vyeti ghushi vya COVID-19 na wakati huo huo, muuguzi huyo pia anakabiliwa na mashtaka mengine 29 ya kuunda vyeti feki.

Alhamisi, Julai 9, 2020, wawili hao walikabiliwa na mashtaka hayo katika mahakama ya Milimani, huku muuguzi huyo akiachiliwa kwa dhamana ya KSh 150,000 na mwenzake akiachiliwa kwa dhamana ya KSh 50,000.

Waziri wa Uchukuzi, James Macharia, alisema wasafiri wanaoingia nchini wanapaswa kuwa na vyeti vinavyoonesha hawana virusi vya COVID-19, na kwa hivyo, watalii hawatalazimika kuingia karantini ya lazima labda tu kama wanaonesha dalili za kuugua maradhi hayo hatari.

Alisema kulegeza kwa masharti hayo kutaipiga jeki sekta ya utalii ambayo imeathirika zaidi na janga hilo la kimataifa.

Wakati huo huo, Katibu katika Wizara ya Afya, Rashid Aman, aliamuru madereva wa matrela kuhakikisha wana vyeti vya kuonesha hawana virusi vya corona hususan wanapovuka mipaka ya Namanga na Busia kuelekea Tanzania na Uganda mtawalia.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →