This archive report was first published on 9 July 2020.
Wavulana wawili wa miaka 6 wameguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na jamaa mmoja aliyewakashifu kwa kumuibia mahindi katika kijiji cha Kiptere.
Chifu wa kata ndogo ya Kiptere David Kipkurui amethibitisha kisa hicho na amesema jamaa huyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Aliposhambulia watoto hao, jamaa huyo alikuwa na kisu na alikuwa akidai kuwa ni njia moja ya kuwaadhibu.
Wakazi wa eneo hilo waliosikia nduru walipata watoto hao wakiwa wamelala sakafuni huku damu ikitiririka.
Alipotekeleza kitendo hicho cha unyama, mshukiwa alijaribu kutoroka lakini alikamatwa na wakazi waliompeleka katika kituo cha polisi cha Sondu ambapo anazuiliwa kwa sasa.