Skip to main content

Nairobi na Mombasa kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya coronavirus

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 9 July 2020.

Nairobi na Mombasa kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya coronavirus

Visa vya Covid-19 vinafikia 8975, na Mombasa ina hatari ya maambukizi zaidi kutokana na kufunguliwa kwa mipaka.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza visa hivyo ikiwa ndio idadi ya juu zaidi kuwahi kuripotiwa tangu kisa cha kwanza mwezi Machi.

Visa hivyo vilitokana na sampuli 3803 ambazo zilifanyiwa ukaguzi.

Waziri Kagwe alisema Mombasa iko katika hatari ya maambukizi zaidi kutokana na kufunguliwa kwa mipaka wa watu wasafiri.

Alisema pia wagonjwa wanne wameangamizwa na makali ya coronavirus.

"Kwa udadisi wetu, ni kama watu 138 kwa sasa wanapatikana na virusi vya Covid-19 kwa kila watu 100,000 Mombasa na watu 100 kwa watu 100,000 Nairobi," alisema Kagwe.

Alionya kuwa Mombasa ina hatari ya maambukizi zaidi kwa sababu watu wengi wamekuwa wakimezea kuzuru eneo hilo baada ya kufunguliwa kwa mipaka.

Alisema visa 1,663 vimeongezeka katika Mombasa na inaweza kuongezeka zaidi kwa sababu Mombasa ni mahali kila mtu wa Nairobi amekuwa akitaka kuzuru.

Waziri Kagwe aliwataka Wakenya kulinda wazee zao wanapoenda mashambani.

Alisema sasa imefikia kiwango cha kila mtu kuhakikisha kuwa anajilinda kikamilifu.

"Sasa katika kila kijiji hapa Mombasa na Kenya nyote, ni wewe tu unaweza kujilinda kikamilifu," alisema Waziri.

Aliwataka wapenzi wa miraa na abiria kuhakikisha wanachukua hatua zifaazo kujilinda.

Aliongeza, "Wale watu wanachonga miraa, hakikisha hauko karibu na mwingine, bado itaingia tu. Wewe chonga ukiwa mbali,".

Waziri aliwataka Wakenya kuwajali wakongwe kwa kuwalinda ifaavyo dhidi ya janga la maradhi hayo.

Alisema, "Mimi nina watoto, nina mama, nina jirani... na mimi pia ni mtoto wa mtu. na ninaweza kumpelekea mamangu nikimkimbilia bila maski,".

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →