This archive report was first published on 9 July 2020.
Wakazi wa mtaa wa Juja, Kiambu waliachwa na mshtuko baada ya dereva wa teksi kupatikana amega dunia karibu na lango la Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) Jumapili, Julai 5.
Alipatikana ameaga dunia ndani ya gari linalotembelea hospitalini, huku taa zikiwa zikiwa zimewashwa. Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, gari hilo lilionekana likiendeshwa kwa kasi kabla ya kupatikana likiwa limeegeswa.
Wakazi walisema gari hilo lilisikika lipiga honi mara kadhaa majira ya saa nane mchana lakini mabawabu wa hospitalini walipuuza wakidhani Maina alikuwa mlevi. Baadaye Maina alionekana ni kana kwamba amelala kwenye kiti cha dereva alichokuwa amekalia.
Ufunguo wa gari na simu yake vilipatikana mfukoni mwake. Mkewe alisema marehemu alitoka nyumbani asubuhi akiwa buheri wa afya, hata hakuwa akipiga chafya.
Charles Chege, nduguye marehemu, alisema zoezi nzima lilizua hofu. Wengi walidhani aliaga dunia baada ya kuugua virusi vya corona.
Alidokeza kuwa mdomo wake ulikuwa umekauka wakati alipatikana ameaga dunia.
Wakazi walimpigia Charles Chege nduguye marehemu wakidhani kuwa ni yeye alikuwa ndani ya gari hilo.