This archive report was first published on 9 July 2020.
Maabara ya hospitali ya Lang'ata ilifungwa ghafla Jumatano, Julai 8, baada ya maafisa wa bodi ya kusimamia maabara nchini kubainisha kuwa haikuwa na vifaa vya kupimia ugonjwa wa COVID-19.
Maafisa wa bodi ya kusimamia maabara nchini (KMLTTB) walifanya msako mkali katika hospitali hiyo na kubaini kuwa haikuwa na vifaa vya kupimia ugonjwa huo.
Maabara hiyo ilikuwa ikiwalipisha wagonjwa KSh 5,500 kwa ajili ya vipimo vya virusi hivyo na kisha sampo zinapelekwa KEMRI kwa majaribio.
Maafisa wa polisi wameanza uchunguzi kufuatia suala huku Mkurugenzi Mkuu wa hospitali huyo na maafisa wengine wa afya wakizuiliwa.
Alisema Patrick Kisabei, afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo, "Kilichotufanya kufunga maabara hiya ni kuwa haina vifaa vya kutumika katika kupima virusi vya corona, hivyo inamaamisha wamekuwa wakiwahadaa wananchi na kuweka maisha yao hatarini."