Skip to main content

Nahodha wa zamani wa timu ya Harambee Stars apona virusi vya corona

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 July 2020.

Mwanasoka wa zamani Musa Otieno alilazwa kwa siku kumi katika hospitali ya Kenyatta baada ya kupatikana na virusi vya corona.

Alipatikana na virusi vya COVID-19 Juni 30, baada ya kufanyiwa vipimo, kwa mujibu wa shemeji yake Collins Okinyo.

Aliyekuwa nahodha wa timu ya kitaifa ya soka Musa Otieno ameruhusiwa kuondoka hospitali baada ya kulazwa kwa siku kumi.

Wachezaji kadhaa wa soka pamoja na Rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa (FKF), kocha wa timu ya Harambee Stars wamemtakia Otieno afueni ya haraka.

Wakenya wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari zinazohitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivi hatari.

Kenya imeripoti visa 8,528 vya maambukizi ya virusi hivyo na vifo 169 vimeripotiwa kwa jumla.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →