This archive report was first published on 8 July 2020.
Usafiri wa treni ya SGR kurejea Jumatatu, Julai 13, baada ya kufungwa kwa siku 7.
Waziri wa Uchukuzi James Macharia alitangaza kuwa treni ya kisasa ya SGR itaanza kufanya safari zake rasmi Jumatatu, Julai 13.
Maafisa 10 watakuwa kwenye treni hiyo wakiwaelekeza abiria jinsi ya kuzingatia amri ya kutokaribiana.
Alisema pia tahadhari zote za kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya COVID-19 yatafuatwa kwa kina.
Usafiri wa treni ya SGR utaanza kwa treni ya kwanza itaondoka jijini Nairobi saa mbili asubuhi na itatarajiwa kufika Mombasa majira ya saa sita na dakika 45 mchana.
Treni hiyo vile vile itaondoka Mombasa saa saba na dakika 25 na inatarajiwa kufika Nairobi mwendo wa saa kumi na mbili na dakika 40.