This archive report was first published on 8 July 2020.
Waziri wa Uchukuzi James Macharia amesema kuwa abiria watakaotua nchini kutoka mataifa ya kigeni hawatalazimishwa kujiweka karantini ikiwa hawataonyesha dalili zozote za ugonjwa hatari wa COVID-19 ambao umeangamiza mamilioni ya watu kote ulimwenguni.
Alisema hii wakati wa kujibu maswali ya wanahabari akiwa katika jumba la Transcom jijini Nairobi, Macharia alisema hatua hiyo inanuia kuwavutia zaidi watalii ikizingatiwa wizara ya Utalii ameathirika sana kufuatia janga la ugonjwa wa Corona.
Abiria watakaowasili nchini watashukishiwa katika maeneo maalumu na la muhumu, na ni sharti wawe na stakabadhi halali.
Wahudumu wa ndege hawatalazimishwa kujiweka karantini endapo joto lao la mwili halitakuwa limezidi nyuzi joto 37.5.
Wizara ya Uchukuzi inaangazia kwamba kufikia sasa, Kenya imerekodi visa 8,528 vya maambukizi ya virusi vya corona huku watu 2,593 wakiripotiwa kupona na vifo 169 kuripotiwa.