Skip to main content

Watu wengine 257 wakutwa na virusi vya COVID-19

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 8 July 2020.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu wengine 257 wamepatikana na virusi vya COVID-19, na jumla ya idadi ya walioambukizwa kufikia 8,528.

Alisema hii akiwa kaunti ya Makueni Jumatano, Julai 8, 2020.

Alisema visa hivyo vilipatikana baada ya sampuli kutoka kwa watu 3,053 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.

Waziri Kagwe pia alisema kuwa kufikia sasa, jumla ya sampuli zilizofanyiwa vipimo kote nchini ni 196,508.

Alisema pia kuwa watu 2,593 wamepona kwa jumla baada ya wengine 89 kuruhusiwa kondoka hospitalini.

Watu waliofariki dunia kutokana na COVID-19 imefikia 169.

Alisema, "Wagonjwa wawili wamefariki kutokana na ugonjwa huu, kwa sasa vifo 169 vimeripotiwa nchini, natuma rambi rambi zangu kwa familia zilizofiwa, ugonjwa huu kwa sasa umekita kambi katika jamii, kaunti zote isipokuwa 5 pekee zimeripoti visa vya maambukizi ya COVID-19, Lazima tuwe macho na tuchukue tahadhari zinazohitajka ili kudhibiti kueneea kwa ugonjwa huu,"

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →