Skip to main content

MaMCA 2 washtakiwa kwa kuwaibia wenzao wakiwa wamejihami Homa Bay

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 8 July 2020.

MaMCA wawili kutoka Kaunti ya Homa Bay, Morris Ogwang' na Michael Odira, walishakiwa kwa madai ya kuwavamia na kuwaibia wenzao wakiwa wamejihami na mawe.

Wawili hao walitekeleza kitendo hicho mnamo Mei 7, 2020, wakiwa wameandamana pamoja na watu wengine eneo la Kendu Bay, Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Kaskazini.

Wawili hao walikuwa wameiba pesa na mali nyingine yenye thamani ya KSh 272,500 kutoka kwa wathiriwa, ikiwa ni pamoja na diwani wa Homa Bay Mjini, Juma Awuor, na mwenzake wa Homa Bay ya Kati, Julius Nyambok.

Awuor aliporwa KSh 75,000, saa ya majira yenye thamani ya Ksh 15,000, na viatu vya thamani ya KSh 2,500, na Nyambok alipoteza KSh 180,000 na kujeruhiwa.

Wakifika mbele ya Hakimu Mkazi wa Homa Bay, Joy Wesonga, wawili hao walikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh150,000 kila mmoja.

Maandamano hayo yalikuwa mnamo Jumanne, Julai 7, 2020.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →