This archive report was first published on 7 July 2020.
Gari la kituo cha polisi cha Navakholo liligonga ukuta wa kanisa Jumatatu, Julai 6, 2020, wakati afisa wa kike alikuwa akifunzwa kuendesha gari na afisa mwenzake wa kiume.
Wakazi wa eneo la Ingotse, Navakholo kaunti ya Kakamega, wanataka adhabu kali ichukuliwe dhidi ya maafisa wawili wa polisi.
Wanashutumu afisa huyo wa kike kwa kusema alikuwa mlevi baada yao kumuondoa ndani ya gari hilo ingawa madai hayo hayangeweza kuthibitishwa.
Wanataka maafisa hao na kituo cha polisi cha Navakholo kwa jumla kuwafidia katika ukarabati wa kanisa hiyo.