This archive report was first published on 6 July 2020.
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kurejelewa kwa safari za ndege nchini kuanzia Agosti 1, 2020, baada ya kufungwa kwa viwanja vya ndege na kupigwa marufuku kuingia na kutoka nchini kwa ndege kwa miezi mitatu na nusu.
Alisema safari za ndege kuingia na kutoka nchini zitaanza huduma kawaida tena, lakini kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Wizara ya Afya na Mamlaka ya safari za ndege.
Uhuru alisema hii wakati akilihotubia taifa Jumatatu, Julai 6, 2020, nje ya jumba la Harambee jijini Nairobi.
Alisema safari za ndege kwenda na kutoka nje mipaa ya Jamhuri ya Kenya zitaanza huduma kuanzia Agosti 1, 2020, pia kwa kufuata mwongozo na masharti ya Wizara ya Afya na Mamlaka ya safari za ndege, na masharti mengine yatakayowekwa kwa wanaotoka na kuingia.
Uhuru alisema hii wakati akilihotubia taifa Jumatatu, Julai 6, 2020, nje ya jumba la Harambee jijini Nairobi.