Skip to main content

Faida za Maji ya Madafu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 July 2020.

Madafu (ngeli ya li-ya) ni nazi changa ambayo haijakomaa, na kwa kuzingatia faida zake, wataalamu wa tiba na dawa asilia huagiza watu kutumia maji ya madafu kwa wingi.

Wanatambua kwamba maji ya madafu yanaaminika kuwa na faida kede kede kwa mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kuzuia upungufu wa maji mwilini na kuimarisha ubongo na misuli.

Wataalamu wa lishe wanashauri maji hayo yanywewe asubuhi kabla ya mtu kutumia chakula au kinywaji chochote, kwani husaidia kupunguza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa kiharusi, kurekebisha kiwango cha sukari katika mwili na kusaidia kurekebisha ngozi na kuponya makovu.

Madafu pia husaidia kuua bakteria wa aina mbalimbali wakiwamo wale wanaosababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo – UTI – kutokana na virutubisho vilivyoko ndani ya maji ya tunda hilo.

Julai 3, 2020, Bw. Ali Bakari akiuza madafu katika eneo la Marikiti, Mombasa. Picha/ Mishi Gongo

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →