Skip to main content

Marafiki wa Uhuru wanataka kujinufaisha na mamlaka yake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 July 2020.

Wandani wa Rais Uhuru Kenyatta wako kwenye mvutano baada ya tofauti kuibuka kati yao.

Alama hizi zimejiri baada ya juhudi za kundi la Kieleweke kuwatimua wandani wa Naibu Rais William Ruto kufaulu.

Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu, ambaye alianzisha mrengo wa Kieleweke, amesema kuna watu wanataka kujinufaisha na mamlaka ya Rais Uhuru Kenyatta.

Wambugu alisema kwa sasa kuna vikundi viwili ndani ya mrengo wa serikali, 'DealMakers na GateKeepers'.

'Kila mfalme ana vikundi hivi viwili, GateKeepers ni watu ambao humfanyia kazi na kuhakikisha wanamlinda na kulinda kazi yake. DealMakers nao ni marafiki wake wa awali kabla awe mfalme. Huwa wanataka kujinufaisha na mamlaka yake kwa ajili ya maslahi yao binafsi,' alisema Ngunjiri.

Wambugu aliongeza, 'Wakati mwingi, vikundi hivi viwili huwa linazozana. Katika siku zijazo, nitakuwa nikielezea nani ni nani.'

Alisema sabbau ya kuanzisha Kieleweke ilikuwa ni kuhakikisha kuwa mamlaka yako kwa Rais pekee lakini sasa kuna marafiki wanaotumia nafasi yao vibaya.

'Mamlaka huwa na mtu mmoja tu. Hayawezi kuwa na watu wawili, hata kama ni marafiki,' alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →