This archive report was first published on 5 July 2020.
Wakati wa kujenga uwezo wa kujilinda dhidi ya Covid-19, Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amewataka Wakenya kujitahidi zaidi kujikinga dhidi ya virusi hivyo.
Alisema hali inayoendelea nchini Marekani na Brazil inafaa kuwa funzo kwa Wakenya kujilinda zaidi dhidi ya janga hilo.
Alisema sekta ya afya italemewa, basi madaktari watalazimika kuchagua ni wagonjwa wapi watawaokoa na watakaoachiliwa wafe.
"Naona madaktari watakuwa wakichagua ni nani atasaidiwa na ni nani atawachwa afe. Tafadhalini hakikisheni mnajiweka salama," alisema Kuria.
Alisema kuna uwezekano mkubwa Rais Uhuru Kenyatta hatafungua nchi kutokana na kuwa maambukizi ya virusi hivyo yanaendelea.
"Kufunguliwa kwa nchi huenda kusifanyike. Labda hata mikahawa itafungwa tena," alisema Kuria.
Aliwataka Wakenya kujua maisha ni yao na wala hawajilindi kwa sababu ya serikali.
Wizara ya Afya Jumamosi, Julai 4 iliripoti visa vingi zaidi vya maambukizi mapya, 389, tangu ugonjwa huo uzuke mwezi Machi.