This archive report was first published on 4 July 2020.
Kamati ya Kuleta Maridhiano Kati ya Waiguru na MCAs Kirinyaga Yaundwa ¶
Kaunti ya Kirinyaga imeunda kamati ya wanachama saba ili kuleta suluhisho la kudumu la mvutano kati ya Gavana Anne Waiguru na wajumbe. Kamati hiyo inajumuisha wazee, viongozi wa kanisa na viongozi wengine wasio wa kisiasa ambao wanatarajia kuleta amani na kuzipatanisha pande hizo mbili.
Kamati hiyo itaandaa mikutano ili kujadiliana na kushauriana na hatimaye kuleta maridhiano kati ya pande hizo mbili. Gavana Waiguru amesema kuwa yuko tayari kwa kamati ya kuleta maridhiano.
Kamati iliyoteuliwa na kuogozwa na mwenyekiti Seneta Cleophas Malala kumpiga msasa na kusikiza malalamishi hayo ilimpata bila hatia. Hata hivyo, kikosi cha Malala kilisema kulikuwepo na uhusiano mbaya wa kikazi baina ya afisi ya gavana na wawakilishi wa wadi.
Kamati hiyo inapendekeza kuandaliwa kwa kikao kati ya Waiguru na bunge la kaunti ili kufanya mashauriano na kurejesha amani miongoni mwao kwa manufaa ya wakazi wa Kirinyaga.
"Kaunti itasalia kuzingatia utoaji wa huduma kwa watu wa Kirinyaga na kukamilisha ajenda ya maendeleo katika miaka miwili ijayo. Tutahakikisha matarajio ya watu wetu yanabaki kuwa lengo la mipango yetu," Waiguru alisema.