This archive report was first published on 4 July 2020.
Alipokuwa gavana wa Nakuru, Kinuthia Mbugua aliteuliwa mtunzi wa Ikulu mwezi Januari 2018 baada ya Rais Uhuru Kenyatta kushinda kipindi cha pili.
Wakati huo huo, bunge la kaunti ya Nakuru lilipendekeza Mbugua achunguzwe kuhusu ufujaji wa KSh 3.5bn.
Ripoti ya kamati ya uhasibu ya bunge hilo inasema KSh 3.5bn zinaarifiwa kutumiwa kwa njia isiyofaa.
Kamati hiyo ilipendekeza EACC ifanye uchunguzi uwezekano wa ukora, wizi na matumizi mabaya ya fedha hizo kima cha KSh 3.5bn.
Ripoti hiyo ilipendekeza Mbugua achunguzwe na tume ya kukabiliana na ufisadi EACC kuhusu fedha hizo kwenye bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2015/16.
Mbugua ndiye alikuwa gavana wa kwanza wa Nakuru kuanzia mwaka wa 2013 kabla ya kubwaga na Lee Kinyanjui.
Kwa sasa anafanya kazi Ikulu kama mmoja wa wapambe wa Rais Uhuru Kenyatta.