Skip to main content

Mabinti wawili wanaswa wakipenyeza bangi katika kituo cha polisi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 July 2020.

Alhamisi, Juni 3, 2020, polisi walikamatwa wawili wa kike waliofichwa bangi katika chupa ya chai wakiwa wanampelekea mshukiwa aliyekuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kirinyaga.

Washukiwa hao wa kike Frida Njeri na Doreen Wambui wenye umri wa miaka 18 na 22 mtawalia walikuwa wanamtembelea James Murithi ambaye alikamatwa kwa ulanguzi wa bangi.

Polisi walisema wawili hao walikamatwa kabla ya kumpa mshukiwa chupa cha chai ambayo walitumia kubeba dawa hizo.

Polisi waliwashurutisha kuifungua chupa hiyo ambayo misokoto ya bangi ilikuwa imefichwa chini yake.

Wawili hao walikuwa wanampeleka mshukiwa aliyekuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi bangi hiyo.

Wambu aliwaambia polisi, "Alituambia tutumie ujanja huo na kumpenyezea bangi hiyo kizuizini kwani hakuwa akijihisi mzima baada ya kuikosa kwa siku mbili,".

Wawili hao wamezuiliwa wakisubiri kufikishwa mahamani.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →