Skip to main content

Umeme Warudishwa Visiwani Pate na Faza Baada ya Majuma Mawili ya 'Kukaa Gizani'

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 July 2020.

Wakazi wa kisiwa cha Faza na Pate walipata raha baada ya majuma mawili ya kukaa gizani kwa sababu ya kukosekana kwa stima eneo hilo. Hali hiyo ilibainishwa na Meneja wa Mauzo wa Kenya Power, tawi la Lamu, Bernard Kataka, ambaye alisema hitilafu za mitambo ya jenereta zilizokuwa zikitumika eneo hilo ziliwahusisha.

Ofisi ya Bw. Kataka ilifanya kazi kwa ufanisi ili kuleta mitambo mipya ili kuhudumia wateja eneo hilo. Mitambo mipya hii ilisaidia kutatua kikamilifu hitilafu iliyokuwa ikishuhudiwa eneo hilo mara kwa mara na kuwataka wakazi kuondoa hofu.

Mapema juma hili, wakazi wa kisiwa cha Faza walishiriki maandamano na kufululiza hadi kwenye ofisi za Kenya Power eneo la Faza kushinikiza kurudishwa kwa stima eneo hilo. Wakazi hao wakiongozwa na Mbunge Mwakilishi wa Wanawake, Bi Ruweida Obbo, walikashifu kampuni hiyo kwa utepetevu katika kushughulikia hitilafu za umeme kila mara zinapotokea eneo la Lamu Mashariki.

“Haya majuma mawili yamekuwa ni kipindi kigumu kwa wakazi wa Faza na Pate, lakini tunawashukuru wateja wetu kwa kutuvumilia hadi tukasuluhisha tatizo,” alisema Bw. Kataka.

“Mimi binafsi nimekuwa nikisukuma bungeni ili visiwa hivi vya Pate na Faza viunganishwe kwa stima. Tulitarajia stima ingekuwa imerudishwa kufikia Juni 27. Hatutaondoka kituoni hapa Faza. Tutalala hapa hadi pale mtakapoturudishia stima,” alisema Bi Obbo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →