This archive report was first published on 2 July 2020.
Kituo cha polisi cha Athi River, kilichopo katika kaunti ya Machakos, Kenya, kimeanzisha uchunguzi baada ya miili ya watoto wawili kupatikana ikioza ndani ya gari lililoegeshwa katika kituo hicho.
Wakati wa kuwasilisha taarifa hii, Juni 2, 2020, Kamanada wa kituo hicho, Catherine Ringera, alisema kwamba watoto hao waliripotiwa kutoweka Juni 11, 2020.
Wawili hao walitoweka mtaa wa KMC wakicheza nje ya nyumba yao, na maafisa wa kituo hicho walisema kwamba ripoti ya kutoweka kwa wawili hao ilipigwa katika kituo hicho na kupelekea kwao kuanza kuwasaka hadi Jumanne, Juni 30, 2020, wakat miili yao ilipopatikana.
Uchunguzi wa kisa hicho unaendelea, na miili ya wawili hao inahifadhiwa katika makafani ya Chiromo baada ya wazazi wao kutambulika.