Skip to main content

DP Ruto: Kuteseka ni kwa muda tu kabla ya Simba wa Yuda kuwasaidia

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 2 July 2020.

Naibu Rais William Ruto amekuwa na kipindi kigumu cha maisha, ikijumuisha hali ngumu ya maisha ya Wakenya wanaopitia janga la coronavirus.

Alhamisi, Julai 2, Ruto alitoa ujumbe wa kuwapa uvumilivu wanaopitia hali ngumu, akisema ni kwa muda tu kabla ya Simba wa Yuda kuwasaidia.

Ujumbe wake ulijiri wakati ambapo Wakenya wanapitia janga la coronavirus huku akipitia mawimbi ya kisiasa.

Ujumbe wake ulizua hisia mseto za kisiasa kutoka kwa wanamtandao wa Tangatanga na Kieleweke.

DP Ruto alinukuu kitabu kitakatifu katika maandiko ya Petro wa kwanza 5:10, ambapo Wakristo wanatakiwa wawe wavumilivu wakati wa mawimbi.

Maandiko ya Petro inawataka wasihofu yote yanayofanyika kwani baadaye anawaahidi kuwa Simba wa Yuda atawaondolea yote.

DP Ruto alisema alikuwa ameshiriki maombi ya asubuhi pamoja na watumishi wa Bwana kutoka kanisa la PCEA na ACK kutoka Mt Kenya wakiongozwa na askofu Charles Muturi.

Ujumbe wake ulizua hisia mseto mara moja kutoka kwa wanamtandao wengi wakichukua mrengo wa kisiasa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →