Skip to main content

Rais Donald Trump asisitiza sio lazima kuvalia barakoa hadharani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 2 July 2020.

Ikizingatiwa kwamba kuna maeneo ambapo watu wameamua kufuata maagizo ya kuvaa barakoa, Rais Donald Trump amesema atakuwa akivalia maski kwa hiari.

Alisema hili wakati wa kujibu maswali kwa shirika la FOX News, na kuongeza kuwa kufunika uso hakuhitaji kuwa suala la lazima katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Trump alisema atakuwa anavalia barakoa katika mazingira yatakamlazimu kufanya hivyo, na kuongeza kuwa anaamini siku moja janga la COVID-19 litatoweka na maisha kurejea kawaida.

Maeneo kadhaa nchini Marekani yanashuhudia ongezeko la maambukizi na vifo kutokana na virusi hivyo, na kufikia sasa, taifa hilo limesajili visa zaidi ya milioni 2.6 vya watu wanaougua homa hiyo na wengine zaidi ya 127,000 wakipoteza maisha yao.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →