This archive report was first published on 1 July 2020.
Wakulima wa eneo bunge la Wundanyi, Tanzania, wamekuwa wakikumbana na tatizo la tumbili wanyama wa porini ambao wamekuwa wakizaana kwa kasi na kuvamia mashamba yao.
Mbunge wa Wundanyi, Danson Mwashako, ameitaka Shirika la Huduma za Wanyama Pori Nchini (KWS) kudhibiti idadi ya tumbili kwa kutumia njia ya upangaji uzazi ili kuzuia ongezeko la idadi ya wanyama hao ambao wanasababisha hasara kwa wakulima wa eneo bunge lake.
Alisema kuwa wanyama hao wa porini wamekuwa wakizaana kwa kasi, kuvamia mashamba na kuwaacha wakulima wakikadiria hasara na kutishia ukulima wa vyakula katika eneo hilo.
“Wenyeji wengi wa eneo hili hutegemea kilimo ili kujikimu kimaisha. Tumbili hawa wamekuwa kero kwa wakulima ambao sasa wamekufa moyo na hivyo kuwacha shughuli za ukulima,” alisema Mwashako kama alivyonukuliwa na Taifa Leo.
Alisema kuwa KWS inatakiwa kuwazia kutumia njia ya kupanga uzazi kudhibiti idadi ya nyani.
Wakulima wa eneo hilo wamekuwa wakikumbana na tatizo la tumbili hao wanyama wa porini ambao wamekuwa wakizaana kwa kasi na kuvamia mashamba yao.
Alisema kuwa juhudi za kutafuta usaidizi kutoka kwa KWS ziligonga mwamba kwani hadi kufikia sasa idara hiyo haijasikia kilio chao.
Wanyama hao ambao hujificha katika milima ya Taita, wamekuwa kidonda sugu kwa wakulima wa Wandanyi licha ya kujaribu kuweka vinyago shambani.
Alilama kuwa juhudi zao za kufikia KWS kwa msaada ziliambulia patupu.
Alisema kuwa Serikali ilitangaza hii majuzi kwamba imetoa fidia ya takriban KSh78 milioni kwa baadhi ya waathiriwa na kuahidi kutenga pesa zingine zaidi za kuwalipa fidia.