This archive report was first published on 1 July 2020.
Eneo la Ainamoi, Jimbo la Kericho, lilikuwa na shambulio la kihisia baada ya mchungaji aliyehusika katika kushiriki uasherati na kimada wake kufumaniwa na mke wake.
Aliondoka nyumbani juzi akimwarifu mkewe alikuwa akienda kuhubiri injili eneo la mbali.
Mkewe akamsindikiza na kumtakia kila la heri, lakini baadaye akapata fununu kuwa mumewe alienda kushiriki uasherati na kimada wake anayeishi mji wa mbali.
Mkewe alitulia nyumbani hadi siku ya kisanga mumewe akarudi nyumbani akiwa na Biblia mkononi huku akiimba wimbo wa injili.
"Nina furaha kuwapata mkiwa salama. Nilifanikiwa kuhubiri injili na watu kadhaa waliokoka," alisema jamaa.
Hata hivyo, mama kwa hasira aliwaka moto akimlaumu jamaa kwa uasherati.
"Acha huo ukora wako! Nimepata habari kamili ulitumia nafasi hiyo kunisaliti na hawara wako. Rudi utokako!" alisema mkewe.
Inasemekana kijogo alishtuka kujua chuma chake ki motoni na akaloa jasho akiwa amekabiliwa na kikohozi.
"Fitina ulizopata zatokana na matendo ya shetani mwenyewe. Achana na hayo na unipe makaribisho ninayostahili," alimwambia lofa.
Maneno ya jamaa yalizua sokomoko zaidi na kumfa ya mkewe kuwika kwa ghadhabu.
Jombi alijua alikuwa amesukumwa kona mbaya na akaamua kupiga magoti kwenye matope na kutoa maombi ya kipekee.
"Naomba mke wangu aone mwanga na asipotoshwe na shetani ili aniache niendeleze huduma," alisali na hasira za kipusa zikapoa ghafla.
"Naye mama watoto alipiga magoti pia na kuomba kuwa Mungu akomeshe tamaa ya ufuska iliyomteka mumewe," alieleza mdaku.
Kisha mke alisema amemsamehe mumewe ambaye naye aliahidi kuwa mwaminifu kwake.