Skip to main content

Afueni kwa wachezaji 2 wa raga waliohukumiwa miaka 15 na kukata rufaa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 1 July 2020.

Wachezaji wawili wa raga walipata afueni baada ya Mahakama Kuu kufuta hukumu ya miaka 15 jela

Wachezaji wawili wa raga, Alex Olaba na Frank Wanyama, walipata afueni Jumanne, Juni 30, baada ya Mahakama Kuu kufuta hukumu ya miaka 15 jela kwa mashtaka ya ubakaji.

Wawili hao walikuwa wamekabithiwa hukumu hiyo na Hakimu Mkuu Martha Mutuku katika mahakama ya Milimani mnamo Agosti 16, 2019, kwa mashtaka ya ubakaji kwa mwanamziki mmoja katika makazi ya Seefar, mtaani Nyayo Highrise, mnamo Februari 10, 2018.

Wawili hao waliwahi kuwakilisha Kenya kupitia timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba, Shujaa.

Wawili hao walipofika mahakamani awali kujibu mashtaka ya ubakaji, walieleza mahakama kupitia wakili wao kwamba mlalamishi aliyekuwa na miaka 24 wakati wa tukio aliamua kulala katika makazi yao kwa sababu ya kulewa chakari na alijaribu kuitisha pesa kutika kwao ili awaondolee lawama lakini walikataa.

Wachezaji hao walikabithiwa hukumu ya miaka 15 jela katika Mahakama ya Milimani, kulingana na kipengee cha 10 cha Sheria za Ubakaji za mwaka 2006.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →